Kwa habari motomoto,
Movie mpyaaa!!
au Comedy za kufa mtu!!
Tafadhali comment kisha weka namba yako
TANGAZO
"Sitaki kutupa muda wangu kujibu kuropokwa na
kelele za Trump," Ayatollah Ali Khamenei alisema
Bw. Trump amekataa kuthibitisha kwa bunge la
Marekani kuwa Iran imetekeleza yaliyo kwenye mkataba huo.
Amatishia kufuta makubaliano yote ya rais Obama .
Trump alitaka mkataba huo kufanyiwa marekebisho
kuizuia Iran kuunda silaha za nyuklia au makombora ya masafa marefu.
Ayatollah Khamenei alisema anakaribisha uungwaji mkono
wa mkataba huo kutoka nchi za Ulaya, lakini akaongeza kuwa ikiwa Marekani
itavunja makubaliano hayo Iran itayatupilia mbali.
Rais Trump pia aliilaumu Iran kwa kuzua misikusuko
nchini Syria, Yemen na Iraq na kukiwekea vikwazo kikosi chenye nguvu nyingi
Iran cha Islamic Revolution Guards Corps.
Sasa bunge la Congress litaamua ikiwa litaiwekea
tena vikwazo vya kiuchumi, ambavyo viliondolewa kama sehemu ya makubaliano
hayo.
Ikiwa hilo litafanyika Marekani itakuwa imekiuka
makubaliano kwenye mkataba huo.
Emoticon Emoticon